Watu Tisa Wakiwemo Watoto Wawili Wamefariki Dunia Na Wengine Zaidi Ya 30 Kujeruhiwa Vibaya Baada Ya Basi La Abiria La Alhabdullilah Linalofanya Safari Zake Kutoka Jijini Dar Kwenda Mtwara Kupinduka Katika Kijiji Cha Mambulu Manispaa Ya Lindi .Ajali Hiyo Iliyotokea Mchana Wa Leo Baada Ya Basi Hilo Kupishana Na Lori Na Kupoteza Mwelekeo Na Kupinduka Hali Iliyochangiwa Na Mvua Kubwa Iliyokua Ikiendelea Kunyesha.Hadi Vyombo Vya Habari Vinatoka Hospitali Marehemu Hao Hawakuweza Kufahamika Kwa Haraka Kutokana Na Kukatika Kwa Viungo Na Tayari Maiti Na Mjeruhi Wote Wamefikishwa Hospitali,Kamanda Wa Polisi Wa Mkoa Lindi George Mwakajinga Ambaye Alikuepo Kwenye Eneo La Ajali Hiyo,Hakuweza Kuongea Chochote Kutokana Na Kutingwa Na Harakati Za Kuokoa Majeruhi Wa Ajali Hiyo |
|
No comments:
Post a Comment