Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kushoto) akizungumza na Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ambapo alimwelezea mikakati ya shirikisho lake katika kuinua kiwango cha mpira wa miguu Tanzania. Mkutano huo umefanyika leo (Januari 20 mwaka huu) ofisini kwa Lowassa jijini Dar es Salaam. |
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema
shirikisho lake limepanga malengo ya muda mfupi na mrefu ikiwa na sehemu ya
mkakati wa kuendeleza na kuinua kiwango cha mchezo huo nchini.
Malinzi
ameeleza mikakati hiyo ya uongozi wake leo (Januari 20 mwaka huu) wakati
alipomtembelea Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ofisini kwake jijini Dar es
Salaam.
Amesema
uongozi wake umepanga malengo hayo ikiwemo kuandaa mashindano maalumu ya
kutafuta vipaji mikoani ili kuondokana na mtindo wa timu ya Taifa (Taifa Stars)
kuundwa na wachezaji kutoka katika klabu chache tu.
Kwa
upande wake Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli ameelezea matumaini yake
kwa uongozi mpya wa TFF katika kuunga mkono juhudi za Rais Jakaya Kikwete katika
kuimarisha na kuinyayua Tanzania katika ramani ya mpira wa miguu duniani.
No comments:
Post a Comment