f

f

RADIO

RADIO
Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Blogger Tips and TricksLatest Tips For BloggersBlogger Tricks
  • NO 1 Banda La Maonesho Ya Sikukuu Ya NaneNane Wilaya Ya Newala | No 2 Wajasiriamali Wakiwa Na Mgeni Rasmi.
  • NO 1.Mgeni Rasmi | No 2 Moja Ya Eneo Linalo Onesha Kilimo Hifadhi.
  • Mabanda Ya Maonesho Ya Sikukuu Ya NaneNane Yalivyopendeza Siku Hiyo Ya Maadhimisho
  • Julius Kambarage Nyerere alizaliwa mwaka 1922 katika kijiji cha Butiama, wilaya ya Musoma, mkoa wa Mara, Tanzania (wakati ule: Tanganyika).....

Thursday, October 17, 2013

PROFESA MUHONGO:WAPOTEZEENI WANAOBEZA BOMBA LA GESI

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amewataka Watanzania kuwapuuza wale wote wanaobeza mradi wa ujenzi wa  bomba la gesi kwani kasi ya utandazaji na uunganishwaji wa mabomba ya hayo unaoendelea. Waziri Muhongo aliyasema hayo wilayani Mkuranga,  wakati wa ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa bomba katika uunganishwaji wa mabomba hayo yanayotarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2014.
Alisema kuwa, ujenzi wa mabomba hayo unaendelea vizuri na kwamba kuna vikosi vitano vinahusika katika ujenzi huo na wengine wanajenga kuanzia Mtwara kuelekea Dar es Salaam na wengine wanaanzia Dar es Salaam kwenda Mtwara ili kukamilisha kilomita 542 za mradi wote.
Waziri Muhongo alisema, mabomba yaliyolazwa  yanayofanyiwa kazi na yatakamilisha kilomita 104, tayari kilomita 34 zimekwisha unganishwa kwa kuchomelewa ikiwa ni hatua ya awali na kwamba kilomita sita zimesilibwa ili kuzuia nafasi ya gesi kuweza kupenya na kupotea.  
Balozi wa China nchini, Lu Youqing, amesisitiza kuwepo na uhuru, urafiki na demokrasia katika kutimiza azma ya kukamilisha ujenzi huo na kwamba kuna uwezekano mkubwa wa mradi huo kumalizika  kabla ya muda uliopangwa kutokana na kasi na juhudi waliyonayo wafanyakazi katika ujenzi huo.
Hii ni mara ya pili kwa Waziri Muhongo na Balozi Youqing kufanya ziara maeneo ambayo ujenzi wa mabomba unaendelea na kwamba wamekubaliana kutembelea maeneo hayo kila mwezi ili kuwapa hamasa wajenzi wawe na kasi  inayotakiwa na hivyo kuwezesha mradi kukamilika kwa wakati.
chanzo: NIPASHE

No comments:

Post a Comment