Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesema kuwa matumaini
ya mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Premier, Manchester United ya
kulihifadhi kombe hilo msimu huu yametumbukia nyongo, baada ya klabu
yake kuishinda United kwa magoli matatu kwa moja.
Nyota wa Cameroon, Samuel Eto'o aliifungia
Chelsea magoli yote matatu na kuandikisha historia yake ya kufunga
magoli matatu katika mechi moja ya ligi kuu ya Premier.'' Ni vigumu sana. Wao wana alama kumi na nne nyuma ya Arsenal, kumi na tatu nyuma ya Manchester City na kumi na mbili nyuma yetu'' Alisema Mourinho. ''Pengine timu moja isambaratike, lakini kwa timu tatu kusambaratika kwa pamoja, itakuwa vigumu sana. Nadhani kilichosalia ni wao kupigania kumaliza katika nafasi za kwanza nne'' Aliongeza Mourinho. Kadi Uwanjani Nahodha wa United Nemanja Vidic alipewa kadi ya njano muda mfupi kabla ya mechi hiyo kumalizika, baada ya kumfanyia madhambi Eden Hazard, naye Rafael da Silve akaonyeshwa kadi ya njano kwa kumjeruhi Gary Cahili dakika moja baadaye. Hata hivyo kocha wa Manchester United, Moyes, alihisa kuwa refa wa mechi hiyo alichukua uamuzi mkali zaidi kwa kuumpa Vidic kadi nyekundu moja kwa moja, huku akikiri kuwa Rafael alikuwa na bahati sana pale refa alimpa kadi ya njano badala ya kadi nyekundu. Naye Mourinho alimsifu Eto'o mwenye umri wa miaka thelathini na mbili, licha ya kuwa aliwahi kumshutumu kuhusiana na matokeo yake hasa baada ya kuwasili kutoka klabu ya Anzhi Makhachkala mapema msimu huu. |
Monday, January 20, 2014
MANCHESTER YATUNDIKWA BAO 3 KWA 1 DHIDI YA CHELSEA
MALINZI AELEZEA MIKAKATI YAKE KWA LOWASSA
Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kushoto) akizungumza na Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ambapo alimwelezea mikakati ya shirikisho lake katika kuinua kiwango cha mpira wa miguu Tanzania. Mkutano huo umefanyika leo (Januari 20 mwaka huu) ofisini kwa Lowassa jijini Dar es Salaam. |
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema
shirikisho lake limepanga malengo ya muda mfupi na mrefu ikiwa na sehemu ya
mkakati wa kuendeleza na kuinua kiwango cha mchezo huo nchini.
Malinzi
ameeleza mikakati hiyo ya uongozi wake leo (Januari 20 mwaka huu) wakati
alipomtembelea Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ofisini kwake jijini Dar es
Salaam.
Amesema
uongozi wake umepanga malengo hayo ikiwemo kuandaa mashindano maalumu ya
kutafuta vipaji mikoani ili kuondokana na mtindo wa timu ya Taifa (Taifa Stars)
kuundwa na wachezaji kutoka katika klabu chache tu.
Kwa
upande wake Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli ameelezea matumaini yake
kwa uongozi mpya wa TFF katika kuunga mkono juhudi za Rais Jakaya Kikwete katika
kuimarisha na kuinyayua Tanzania katika ramani ya mpira wa miguu duniani.
HIVI NDIVYO WATU 13 WALIVYOPOTEZA MAISHA PAPO HAPO KUFUATIA AJALI MBAYA YA NOAH NA LORI LEO MKOANI SINGIDA
Kamanda
wa polisi mkoa wa Singida, SACP Geofrey Kamwela, akitoa taarifa ya
ajali ya Noah T.730 BUX kuongwa na Lori aina ya Scania T.687 AXB katika
barabara kuu ya Singida- Dodoma eneo la kijiji cha Isuna tarafa ya
Ikungi wilaya ya Ikungi.Abiria 13 waliokuwa kwenye Noah wamefariki dunia
na watatu wamepata majeraha madogo madogo.Ajali hiyo imetokea
leo.(Picha na Gasper Andrew).
(KUMRADHI KWA PICHA WADAU).Baadhi
ya wakazi wa kijiji cha Isuna tarafa ya Ikungi wilaya ya Ikungi mkoa wa
Singida, wakitoa miili ya abiria wa Noah T.730 BUX waliofariki baada ya
gari hilo kugongwa na lori aina ya Scania T.687 AXB kwenye barabara kuu
ya Singida – Dodoma leo. Noah hiyo ilikuwa ikitoea Itigi wilayani
Manyoni akienda Singida mjini.(Picha na Nathaniel Limu).
ABIRIA
13 wakiwemo watatu wa familia moja wamefariki dunia mkoani Singida leo,
baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Noah T.730 BUK, kugongwa
na Lori aina ya Scania.
Ajali
hiyo ya kusikitisha imetokea leo saa 1.32 asubuhi katika barabara kuu
ya Singida-Dodoma eneo la kijiji cha Isuna tarafa ya Ikungi wilaya ya
Ikungi mkoani Singida.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Singida,SACP ,Geofrey Kamwela, amesema gari hilo aina
ya Noah lilikuwa likitokea Itigi wilaya ya Manyoni na lilikuwa na
safari ya kuja Singida mjini.
Amesema
hadi sasa miili ya abiria 10 wamekwisha tambuliwa na ndugu zao na miili
ya abiria watatu,bado haijatambuliwa na miili yote bado imehifadhiwa
kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa mjini Singida
Alitaja
waliotambuliwa na makazi yao kwenye mabano kuwa ni Omari Shaban (44) na
mke wake Salma Omari na mtoto wao Nyamumwi Omari (10) wote wakazi wa
Itigi mjini.
Kamwela
alitaja wengine kuwa ni Haji Mohammed (29) (Msisi),Mtunku Rashidi (68)
(Sajaranda),Salehe Hamisi (28) (Sajanranda),Samir Shaban (20)
(Puma),Mwaleki Nkuwi (35) (Ikungi),Athumani Kalemba (38) na Ramadhan
Mkenga (Sajaranda).Katika ajali hiyo,abiria watatu walinusurika na
kupata majeraha madogo madogo.
Amefafanua
juu ya ajali hiyo,Kamanda huyo alisema kuwa lori aina ya scania T.687
AXB wakati likipishana na noah,lilihama upande wake na kuifuata noah
ambayo ilikuwa upande wake wa kushoto,na kuligonga na kisha kuliburuza
kati zaidi ya 15.
“Kwa
sasa bado hatujajua chanzo cha ajali hiyo mbaya ingawa baadhi ya watu
wanadai kuwa huenda dereva wa lori alisisia na kusababisha lori hilo
kuhama upande wake na kufuata noah.Uchuguzi utakapokamilika,tutatoa
taarifa hiyo”,amesema.
Wakati
huo huo,mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa mjini Singida,Dk.Banuba
Deogratius amekiri kupokea miili ya abiria hao 13 na kusema kati
yao,watoto ni wawili.habari kwa hisani ya moblog.
RAIS KIKWETE ATEUA MAKATIBU TAWALA WAPYA MIKOA MITANO NA KUHAMISHA WENGINE WAKIWEMO WAKURUGENZI WA MAJIJI
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 |
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O.
BOX 9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA UMMA
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo,
Jumamosi, Januari 18, 2014, amefanya
uteuzi wa Makatibu Tawala wapya wa mikoa mitano na kuhamisha makatibu tawala
wengine na Wakurugenzi wa Majiji nchini.
Taarifa
ya Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue iliyotolewa jioni ya leo,
Ikulu, Dar Es Salaam inasema kuwa uteuzi na uhamisho huo unaanza leo hii.
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo, Makatibu Tawala
wapya ni Ndugu Wamoja A. Dickolangwa ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa
Mkoa wa Iringa ambako alikuwa Kaimu Katibu Tawala; Ndugu Abdallah D. Chikota
ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi. Kabla ya hapo, alikuwa
Mkurugenzi wa Halmashauri wa Wilaya ya Newala na Ndugu Symthies E. Pangisa
ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa. Kabla ya uteuzi wake,
Ndugu Pangisa alikuwa Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara.
Wengine
ni Ndugu Alfred C. Luanda ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa
Mtwara. Kabla ya uteuzi wake, alikuwa
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora na Ndugu Jackson L. Saitabau
ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe. Kabla ya hapo, alikuwa
Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Arusha.
Taarifa
hiyo iliwataja waliohamishwa kuwa ni Ndugu Beatha Swai aliyekuwa Katibu Tawala
wa Mkoa wa Pwani na sasa anahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI; Ndugu
Sipora J. Liana ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha anahamishiwa Ofisi
ya Waziri Mkuu, TAMISEMI; Ndugu Benedict Ole Kuyan ambaye alikuwa Katibu Tawala
wa Mkoa wa Tanga anahamishiwa Mkoa wa Mara na Ndugu Salum M.Chima ambaye
alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa anahamishiwa Mkoa wa Tanga.
Wengine
waliohamishwa ni Ndugu Mgeni Baruani ambaye alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa
Njombe anahamishiwa Mkoa wa Pwani; Ndugu Juma R. Iddi ambaye alikuwa Mkurugenzi
wa Jiji la Mbeya anahamishiwa Jiji la Arusha kama Mkurugenzi; Eng. Omari Chambo
ambaye alikuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi anahamishiwa Mkoa wa Manyara
kama Katibu Tawala wa Mkoa huo na Dkt. John Ndunguru aliyekuwa Naibu Katibu
Mkuu, Wizara ya Ujenzi anahamishiwa Mkoa wa Kigoma kama Katibu Tawala wa Mkoa
huo.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
AJALI MBAYA YAUA 9 NA KUJERUHI 30 MKOANI LINDI
JAMBAZI LAUA NEWALA
Jeshi
la Polisi mkoani Mtwara linamsaka mtu mmoja ambaye hajatambuliwa jina
kwa tuhuma ya ujambazi na mauaji mwananchi mmoja na afisa upelelezi wa
jeshi hilo wilayani Newala ASP Nurdin Kassim Seif.
Mwananchi mwingine aliayeuawa katika shambulio hilo la kustukiza ametambuliwa kuwa ni Hamza Msangaluwa aliykufa hapohapo na askari aliyetambuliwa kwa jina Robert Isaya (33) amejeruhiwa vibaya majani na amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Newala.
Taarifa lliyotolewa na jeshi hilo na kusambazwa kwa vyombo vya habari mkoani Mtwara inasema mtu huyo akiwa na siraha aina ya SMG alifika katika kituo cha kuuzia mafuta cha camel katika kijiji cha Kiduni nje kidogo ya mji wa Newala na kuwalazimisha wahudumu kutoa fedha za mauzo yote ya siku mbili kwa kuwatishia na silaha.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyosainiwa na kaimu kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mtwara Issa Mnilota jambazi huyo alifanikiwa kupora kiasi cha zaidi ya shs 3,299,180 ndipo wananchi walipojitokeza kumfukuza hadi umbali wa kiliomita 8 kabla ya jeshi la polisi kufika katika eneo la tukio.
Taarifa inabaisha kuwa maofisa wa jeshi la polisi walpofanikiwa kufika katika eneo la tukio mtuhumiwa akiwa amejificha vichakani alifyatua risasi na kuumuua raia papo hapo na baadaye kabla ya kumshambulia aliyaekuwa afisa upelelezi wa wilaya ya Newala na kusababisha kifo chake.
Mwili wa marehemu Hamza umekwishachukuliwa na ndugu zake kwa ajili ya taratibu za mazishi wakati ule wa ASP Nurdin Kasim Seif bado umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Newala kusubiri taratibu zingine.
Jeshi la polisi linatoa shukrani kwa wananchi wilayani Newala kwa ushirikisno waliouonyesha na kuendelea kutoa wito kwa wananchi mkoani humo kuendelea kushirikiana katika kuwabaini na kuhakikisha wale wote waliohusika wanatiwa nguvuni.
Mwananchi mwingine aliayeuawa katika shambulio hilo la kustukiza ametambuliwa kuwa ni Hamza Msangaluwa aliykufa hapohapo na askari aliyetambuliwa kwa jina Robert Isaya (33) amejeruhiwa vibaya majani na amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Newala.
Taarifa lliyotolewa na jeshi hilo na kusambazwa kwa vyombo vya habari mkoani Mtwara inasema mtu huyo akiwa na siraha aina ya SMG alifika katika kituo cha kuuzia mafuta cha camel katika kijiji cha Kiduni nje kidogo ya mji wa Newala na kuwalazimisha wahudumu kutoa fedha za mauzo yote ya siku mbili kwa kuwatishia na silaha.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyosainiwa na kaimu kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mtwara Issa Mnilota jambazi huyo alifanikiwa kupora kiasi cha zaidi ya shs 3,299,180 ndipo wananchi walipojitokeza kumfukuza hadi umbali wa kiliomita 8 kabla ya jeshi la polisi kufika katika eneo la tukio.
Taarifa inabaisha kuwa maofisa wa jeshi la polisi walpofanikiwa kufika katika eneo la tukio mtuhumiwa akiwa amejificha vichakani alifyatua risasi na kuumuua raia papo hapo na baadaye kabla ya kumshambulia aliyaekuwa afisa upelelezi wa wilaya ya Newala na kusababisha kifo chake.
Mwili wa marehemu Hamza umekwishachukuliwa na ndugu zake kwa ajili ya taratibu za mazishi wakati ule wa ASP Nurdin Kasim Seif bado umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Newala kusubiri taratibu zingine.
Jeshi la polisi linatoa shukrani kwa wananchi wilayani Newala kwa ushirikisno waliouonyesha na kuendelea kutoa wito kwa wananchi mkoani humo kuendelea kushirikiana katika kuwabaini na kuhakikisha wale wote waliohusika wanatiwa nguvuni.
Subscribe to:
Posts (Atom)