Mhe. Mkuchika akiwasomea wananchi wa kijiji cha Mdenga yaliyoandikwa katika Cheti cha Kijiji hicho kabla ya kukikabidhi kwa Mwenyekiti wa Kijiji. |
Ziara
hiyo ilianza tarehe 30/09/2013 mpaka tarehe 04/10/2013 na ilihusisha vijiji
ishirini (20) ambavyo ni Namangudu, Mdenga, Mahoha, Bahati, Likwaya, Chiwinda,
Nandwahi, Kitangari, Tulieni, Matale, Namkonda, Mitahu, Mapili, Chikwedu,
Mnalale, Matokeo, Mandumba, Kilidu, Mtangalanga na Butiama.
Mh.
Mkuchika aliambatana na wakuu wa idara kutoka halmashauri ya wilaya ya newala,
mkuu wa wilaya ya newala na viongozi wa chama cha mapinduzi wa wilaya hiyo ili
kuongea na kujibu kero za wananchi. Viongozi alioambatana nao kutoka halmashauri
ya wilaya ya newala ni Afisa Utumishi Bw. George Mussa; Kaimu Mhandisi wa Maji
Bw. Nsajigwa Sadiki; Afisa Habari Bi. Lilian Lundo na Bi. Joseline Chambasi;
Kaimu Mhandisi wa Ujenzi Bw. Albano Chilwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri
Wilaya ya Newala Bw. Meggah Ramadhani. Pia aliambatana na mkuu wa wilaya ya
newala Bw. Christopher Magalla pamoja na viongozi wa Chama cha Mapinduzi ambao ni
Mwenyekiti wa CCM wilaya Bw. Ally Sadi; Makamu Mweyekiti Bw. Dadi .S. Kubanga;
Mwenyekiti umoja wa wanawake (U.W.T) wilaya Bibi. Suwabu Msoweta; Katibu umoja
wa vijana wilaya Bw. Andrea Gwaje; Katibu mwenezi Bw. Juma Limonga ; na Mwenyekiti
kamati ya siasa wilaya Bw. Namata .A. Namata.
Pia Mh. Mkuchika alitumia ziara hiyo kufungua
rasmi na kutoa vyeti vya usajili wa vijiji vipya; kuwashukuru wananchi kwa
kuendelea kuwa na imani na chama tawala
(CCM); kuwakumbusha wananchi umuhimu wa kudumisha amani na mshikamano;
kusisitiza umuhimu wa kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (bima ya afya) na
kuzingatia maendeleo ya wilaya.
Vijiji
vipya vilivyofunguliwa rasmi pamoja na kukabidhiwa vyeti na mh. mkuchika ni pamoja na Mdenga; Likwaya; Chiwinda;
Tulieni; Mbebede; Matale; Chikwedu; na Mnalale.
Mh.
Mkuchika alisema kufungua vijiji vipya ni moja ya sera ya serikali katika
kugawanya maeneo ya utawala ili kusogeza huduma karibu na wananchi.
No comments:
Post a Comment