Mtaalamu Mshauri wa Mpango wa kunusuru kaya masikini unaoendeshwa
na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchni TASAF
Rogelio Gomez Hermosillo akiwa katika kikao cha kujadili zoezi la
utambuzi wa kaya masikini katika wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara.
Mfuko
wa Maendeleo ya Jamii TASAF umeanza kazi
ya kutambua kaya masikini na zinazoishi katika mazingira hatarishi nchini kazi
iliyoanza katika mikoa ya Mtwara na Lindi baada ya majaribio kufanyika katika
wilaya za Bagamoyo,Kibaha,Chamwino na Bunda kuonyesha mafanikio makubwa, zifuatazo ni baadhi ya shughuli zilizofanywa
na Mtaalamu Mshauri wa Mpango huo kutoka Benki ya Dunia ROGELIO GOMEZ HERMOSILLO aliyefanya ziara ya
kuona namna kazi hiyo inavyoendelea mkoani Mtwara.
Baadhi
ya wawezeshaji katika mpango wa kunusuru kaya masikini unaoratibiwa na Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii TASAF wakiwa katika kikao
cha pamoja na Mtaalamu Mwelekezi kutoka Banki ya Dunia Rogelio Gomez Hermosillo ( hayupo pichan)ikatika
hafmashauri ya Masasi Mikindani.
Mtaalamu Mshauri wa Mpango wa kunusuru Kaya
Masikini unaoendeshwa na TASAF Awamu ya
TATU Rogelio Gomez Hermosillo akizungumza
na walengwa wa mpango huo katika mtaa wa Chuno
Manispaa ya Mtwara Mikindani juu ya umuhimu wa kutekeleza zoezi la
utambuzi wa kaya masikini kwa uangalifu mkubwa.
Mtaalam wa Mafunzo na Ushiriki wa
TASAF Bi.Mercy Mandao Mariki akifafana jambo kwa walengwa
wa Mpango wa kunusuru kaya masikini katika Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Mtaalamu wa Mafunzo kutoka TASAF Bi Mercy
Mandao Mariki akifafanua jambo kwa Mtaalamu Mwelekezi wa Mpango wa kunusuru
kaya masikini kutoka Benki ya Dunia Rogello Gomez Hermosillo
walipotembelea walengwa wa Mpango huo latika halmashauri ya wilaya ya Masasi
mkoani Mtwara kuona namna kazi ya kutambua kaya masikini inavyoendelea.
Baadhi ya walengwa wa Mpango wa kunusuru
kaya masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF wakishiriki
kazi ya utambuzi katika eneo la Chuno
Manispaa ya Mtwara Mikindani Mkoani Mtwara..
Wawezeshaji Ngazi ya halmashauri ya wilaya
ya Masasi mkoani Mtwara wakimsikiliza Mtaalamu Mwelekezi wa Mpango wa kunusuru
kaya masikini kutoka Benki ya Dunia Rogello Gomez Hermosillo (hayupo pichani) juu
ya namna ya kutambua kaya za walengwa wa
mpango huo ulioanza kutekelezwa katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Mtaalam
Mshauri wa Mpango wa kunusuru kaya
masikini kupitia Mafuko wa Maendeleo ya Jamii nchini TASAF Rogelio
lGomez Hesmosillo aliyeshika tama akisikiliza mchango wa mmoja
wa wawezeshaji wa mpango huo(hayupo
pichani) wakati wa mjadala wa namna
zoezi la utambuzi wa kaya masikini katika halmashauri ya Mtwara Mkindani
mkoani
Mtwara linavyoendelea.
No comments:
Post a Comment